×

Haaland kuongoza Man City dhidi ya Sunderland EPL leo

Manchester City itakuwa mwenyeji wa Sunderland jioni ya leo Jumapili, Septemba 20, katika mchezo wa Ligi Kuu England utakaochezwa kwenye Uwanja wa Etihad. Mchezo huo utaanza saa 16:00 jioni, ukiwa ni mchezo wa raundi ya tano ya EPL msimu wa 2026/27.

Manchester City wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na mwanzo mzuri wa msimu, baada ya kushinda michezo yote minne ya kwanza ya EPL na kukusanya pointi 12. Katika mchezo wao uliopita wa ligi, walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United kwenye dimba la Old Trafford, huku Erling Haaland akifunga bao pekee la mchezo huo.

Kwa upande wa Sunderland, timu hiyo imekusanya pointi nne katika michezo minne ya mwanzo, ikishinda mmoja, sare mmoja na kupoteza miwili. Mchezo wao uliopita wa ligi uliisha kwa sare ya 1-1 dhidi ya Brentford, kabla ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya AZ Alkmaar katika Europa League katikati ya wiki.

Haaland anatarajiwa kuwa mchezaji wa kuangaliwa zaidi katika mchezo huo kutokana na kuanza msimu akiwa na mabao manne katika mechi nne za ligi.

Taarifa za ratiba, matokeo na takwimu za michezo mbalimbali ya EPL zinapatikana kupitia majukwaa ya taarifa za michezo, ikiwemo Meridianbet, pamoja na vyanzo vingine vya michezo.

Manchester City Pia wana wachezaji wenye uwezo wa kutengeneza nafasi kama Anthonio Semenyo na Rayan Cherki, wakati Sunderland watategemea wachezaji kama Granit Xhaka, Enzo Le Fée na Wilson Isidor katika kujaribu kuvunja  safu ya ulinzi ya Mn city.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, hasa kutokana na Sunderland kuhitaji matokeo mazuri dhidi ya moja ya timu zinazoshika nafasi za juu. Manchester City, kwa upande wao, watajaribu kutumia faida ya kucheza nyumbani na kuendeleza mwenendo wao mzuri katika msimu huu.

Leave a Comment