×

Makamu wa Rais Afanya Ziara ya Kushtukiza Arusha – Picha

ARUSHA: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amefanya ziara ya kushtukiza katika Jiji la Arusha, akitembea katika mitaa mbalimbali huku akisalimiana na wananchi na kujionea hali ya mazingira.

Makamu wa Rais alifanya matembezi hayo wakati akielekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru, ambako alifanya ziara ya kushtukiza kwa ajili ya kukagua huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Akiwa njiani, Ndejembi alizungumza na wananchi mbalimbali waliokutana naye, huku akijionea hali ya usafi na mazingira katika maeneo aliyopita.

Baada ya kuwasili Hospitali ya Mount Meru, Makamu wa Rais alikagua huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapo na kuzungumza na wagonjwa pamoja na watumishi kuhusu hali ya huduma na changamoto zinazowakabili.

Ziara hiyo imefanyika ikiwa sehemu ya jitihada za viongozi kujionea hali halisi ya huduma na mazingira wanayoishi wananchi, bila kutegemea taarifa za kiutendaji pekee.

Leave a Comment