
Wanandoa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Zuchu, wamepokea wageni wao maalumu, staa wa muziki kutoka Nigeria, David Adedeji Adeleke ‘Davido’, pamoja na mkewe Chioma, nyumbani kwao Mbezi jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, wawili hao walipata nafasi ya kukutana na kufurahia muda pamoja na Diamond na Zuchu, ambapo pia walishiriki chakula katika mazingira ya kifamilia.

Aidha, Diamond na Zuchu walipata fursa ya kuwaonyesha wageni wao mtoto wao, jambo lililoongeza ladha ya ukaribu na urafiki kati ya familia hizo mbili za mastaa wa muziki Afrika.
Mapokezi hayo yanaonyesha ukaribu uliopo kati ya wasanii hao wakubwa kutoka Tanzania na Nigeria, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakihusishwa na ushirikiano na mahusiano mazuri katika tasnia ya muziki wa Afrika.

Davido ni miongoni mwa majina makubwa katika muziki wa Afrobeats duniani, huku Diamond Platnumz akiwa miongoni mwa wasanii waliochangia kwa kiasi kikubwa kuutangaza muziki wa Tanzania kimataifa.
Kutembeleana kwa mastaa hao kunazidi kuonyesha namna muziki unavyoweza kujenga urafiki na mahusiano nje ya mipaka ya nchi zao.


