Kampuni ya Xiaomi Tanzania imeongeza msisimko katika msimu huu wa Black Friday kwa kuanzisha kampeni maalumu ya kuwazawadia wateja wake nchini, ambapo wanunuzi wa simu teule za REDMI watanufaika na zawadi mbalimbali za bure pamoja na bando la intaneti la GB 96 kutoka Vodacom.
Kampeni hii inayotarajiwa kuendelea hadi 30 Novemba 2026, inalenga kuwapa wateja thamani zaidi wanaponunua simu zao, huku ikiwawezesha kufurahia teknolojia bunifu za REDMI pamoja na zawadi za kipekee.
Kupitia kampeni hii, wateja watakaonunua simu za REDMI zinazostahili kupitia maduka ya mawakala washirika wa Xiaomi nchini kote watanufaika na zawadi maalumu kulingana na aina ya simu watakayonunua.
ZAWADI ZA KIPEKEE KWA KILA UNUNUZI
Katika kampeni hii ya Black Friday, Xiaomi imeandaa zawadi mbalimbali kwa wateja wake kulingana na aina ya simu watakayonunua kama ifuatavyo:
• Ukinunua REDMI A7: Unapata kikombe bure.
• Ukinunua REDMI A7 Pro: Unapata chupa ya maji bure.
• Ukinunua REDMI 17: Unapata mwavuli bure.
• Ukinunua simu yoyote ya REDMI Note 17 Series: Unapata zawadi maalumu ya REDMI Watch 6 Active (Smartmatch) Bure…
Mbali na zawadi hizo, kila mteja atakayenunua simu ya REDMI inayostahili kupitia maduka ya mawakala washirika atapata pia BANDO LA GB 96 BURE KUTOKA VODACOM. Ofa hii inalenga kuwawezesha wateja kufurahia zaidi huduma za kidijitali, ikiwemo matumizi ya mitandao ya kijamii, kutazama video, kusikiliza muziki, kuperuzi mtandaoni na kuwasiliana na ndugu na marafiki.
BETRI KUBWA KWA MATUMIZI YA MUDA MREFU ZAIDI
Katika msimu huu wa Black Friday, Xiaomi pia inaendelea kuonyesha ubunifu wake katika teknolojia ya simu janja, hususan katika uwezo wa betri unaowawezesha watumiaji kufanya shughuli zao kwa muda mrefu zaidi.
Simu mpya za REDMI Note 17 Series zinakuja na uwezo mkubwa wa betri unaolenga kukidhi mahitaji ya watumiaji wanaotegemea simu zao kwa shughuli mbalimbali za kila siku.
REDMI Note 17 inakuja na betri kubwa ya 7,700mAh, inayowezesha matumizi ya muda mrefu kwa shughuli mbalimbali ikiwemo mawasiliano, burudani na matumizi ya intaneti.
Kwa upande mwingine, REDMI Note 17 Pro Max inakuja na betri kubwa zaidi ya 10,000mAh, ikiwa chaguo kwa watumiaji wanaohitaji simu yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi chaji kwa muda mrefu.