×

Omog: Tutachukua Makombe Matatu Msimu Huu

omog

Simba wakiendelea kufanya mazoezi na Kocha wao Joseph Omog.

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam Championi Jumatano Toleo na 1955

KOCHA Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, amesema anaamini watachukua makombe matatu msimu huu kutokana na ubora wa kikosi chake ulivyo hivi sasa.

simba-sc

Kikosi cha timu ya Simba.

Akizungumza na Championi Jumatano, Omog alisema kuwa mwendo ambao Simba imekuwa ikienda nao katika mechi zake za Ligi Kuu Bara, ndiyo huohuo itakaoenda nao kwenye michuano hiyo.
“Kikubwa kwetu ni ushindi, haijalishi tumefunga mabao mangapi, hata kama tukifunga bao moja lakini ilimradi tu tuwe tumeshinda na kuondoka na pointi tatu.
“Tukifanya hivyo katika mechi zetu zote, basi ubingwa utakuwa wetu na ni matumaini yetu kuwa hilo litatimia kwa sababu kikosi changu kwa sasa kipo vizuri na ninataka kombe hili (Mapinduzi Cup) ndilo liwe la kwanza kwetu kulipata msimu huu kisha lile la Ligi Kuu Bara na baadaye la FA,” alisema Omog na kuongeza:
“Hakuna timu yoyote tunayoiogopa ila tutapambana katika mechi zetu zote hata kama tutakutana na Yanga huko mbele.”

Waone Wolper na Harmonize Wakidendeka Live Jukwaani