
Lulu Abas ‘Lulu Diva’
Stori: Mayasa Mariwata | RISASI
MWANADADA anayechipukia katika Bongo Fleva, Lulu Abas ‘Lulu Diva’ amesema hana papara ya mafanikio ya kimuziki kwa vile fani hiyo ipo katika damu.

Lulu Abas ‘Lulu Diva’
Akipiga stori na Risasi Vibes, msanii huyo anayetamba na Wimbo wa Milele aliomshirikisha Elias Barnaba, alisema wasanii wengi wanapoingia kwenye muziki huwa wana kiherehere cha kunufaika haraka, jambo ambalo halipo kichwani kwake kwani kwa sasa muziki bado haujaanza kumlipa.
“Kilichonisukuma ni mapenzi ya dhati na hii fani, si mambo ya mkwanja, kitendo cha kuitwa msanii wa muziki ni furaha tosha kwangu kutimiza ndoto yangu ya tangu utotoni, ndiyo maana sina haraka ya mafanikio kupitia muziki, najua unalipa ila kwangu bado, sina presha hiyo” alisema.