MWANAMUZIKI wa miondoko ya Hip Hop Bongo, P The MC anayetamba na ngoma iitwayo Run DSM aliyomshirikisha Young Killer na Dully Skyes, amefunguka kuwa ameshindwa kuachia wimbo wake mpya kwenye media na mitandao ya kijamii hivi karibuni kufuatia kuchelewa kwa video ya wimbo huo unaoitwa Mambo Leo aliopanga kuuachia hivi karibu aliomshirikisha Mwanamuziki Nandy.
Rapa huyo ameiambia Uwazi Showbiz kuwa licha ya wimbo huo kukamilika anahofia kuuachia bila video ili usije ukashindwa kufanya vizuri kama zilivyo baadhi ya nyimbo zake alizoziachia huko nyuma.
“Wimbo upo tayari lakini siwezi kuuachia hewani bila video, unaweza kupotelea juu kama ilivyo kwa nyimbo nilizofanya huko nyuma, kwa sasa nipo katika taratibu za kufanya video zikikamilika nitaachia kila kitu kwenye media,” alimaliza P The MC.
Kwa stori zote kali, Tu-follow
Facebook @Globalpublishers
Twitter @GlobalHabari
Instagram @GlobalPublishers
YouTube @GlobalTVTZ
UWAZI