The House of Favourite Newspapers

Mali za Kanumba Apewa ‘Pacha’ Wake

Fred Swai (Pacha wa Kanumba) na Flora Mtegoa (Mama Kanumba)

Na MAYASA MARIWATA| GAZETI LA AMANI| SHOW BIZ XTRA

KATIKA hali isiyotarajiwa mama wa staa asiyechuja Bongo, marehemu Steven Kanumba Flora Mtegoa ameamua kumpa mikoba ya msanii huyo kijana aliyemtambulisha kuwa ndiye mrithi wa mwanaye, msanii wa Igizo la Dhamira, Fredy Swai.

Tukio hilo lilijiri Alhamisi iliyopita nyumbani kwa mama huyo maeneo ya Kimara Temboni Dar ambapo aliamua kumkabidhi mikoba ya Kanumba kijana huyo, kutokana na msimamo wake kuwa, kwa jinsi alivyofanana na mwanaye ana kila sababu ya kumthamini kwa kuwa ndiyo faraja ya pekee aliyonayo sasa.

Marehemu Steven Kanumba
Fred na Kanumba

Katika tukio hilo ambapo Fredy alitakiwa kupiga goti, kisha akamkabidhi gitaa, scripti,kitabu kiitwacho Kanumba The Great Fallen Tree na viatu vitu ambavyo mama Kanumba alikuwa akivitunza kama kumbukumbu na kugoma kumpa mtu yeyote hata ndugu zake, kisha akamfanyia maombi mafupi kumbariki katika safari ya kutembelea nyota ya staa huyo.

Marehemu Kanumba

“Nimeamua kumpa mikoba ya Kanumba huyu Fredy sababu nimeshampitisha kuwa ndiye mrithi wa mwanangu, tangu kijana wangu afariki huu mwaka wa tano sijawahi kumkubali kumpitisha wala kumpa Baraka mtu yeyote aliyejiita Kanumba, nimeamua kwa moyo mmoja kumpokea kijana huyu sababu ni faraja kubwa kwangu.

“Nimeenda kuonana na wazazi wake kuwaeleza jinsi nilivyofarijika kujuana naye, nimsihi tu atumie ubunifu wake kukuza sanaa ili asiharibu cv ya Kanumba na asije akanidharau kama wengine waliokuja kwa magoti nikawasafisha kwenye jamii, leo imekuwa majuto kwangu,” alisema mama huyo huku akimpiga kijembe staa wa filamu Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’.

 

Comments are closed.