The House of Favourite Newspapers

Q Chillah: kwenye Hili la Mkataba Mbona Kuna Sintofahamu?

Q Chief

Na OJUKU ABRAHAM| GAZETI LA IJUMAA|ZA CHEMBE

Q Chief ndilo jina alilokuja nalo katika muziki, miaka ile ya mwanzoni kabisa mwa 2000, alipoibuka na ile singo yake ambayo itaendelea kubaki katika orodha ya nyimbo bora kabisa kuwahi kutokea katika Bongo Fleva, Si Ulinikataa!

Ndipo watu walipoanza kuona tofauti za sauti na jinsi watu walivyojaaliwa kuwa nazo katika game. Wakapata namna ya kuweza kumlinganisha na TID au Dully Sykes, ukiachana na sauti ya kubembeleza aliyokuwa nayo Joslin.

Q Chief na T.I.D

Tangu wakati huo, Q Chief ambaye baadaye alitaka mashabiki wamtambue kama Q Chillah alibakia kuwa alama ya muziki huu, ambao leo umekutana na sauti nyingi nzuri, kama za akina Ali Kiba, Barnaba, Ben Paul na chipukizi wengine wengi wa kizazi hiki.

Unapomzungumzia Q Chillah, unamzungumzia mmoja wa wasanii wanaojua nini wanafanya wanapokuwa nyuma ya kipaza sauti, namna anavyoingiza kazi zake na hata anavyochangamka anapokuwa jukwaani.

Ni vile tu upepo mbaya ulimpitia miaka michache iliyopita, alipokutana na majaribu ya matumizi ya madawa ya kulevya, kidogo nusura apotee, lakini jambo la kumshukuru Mungu ni kuwa alishtuka, akalazimisha kujiondoa na sasa ni mtu mwema tena katika sanaa.

Kama siyo jaribu hilo, ukweli ni kwamba huyu angeendelea kuwa juu katika muziki kama walivyo wakongwe wachache ambao wamejibakiza katika chati licha ya upinzani mkali kutoka kwa chipukizi wenye njaa ya mafanikio katika Bongo Fleva.

Huu ulikuwa ni mgodi unaotembea, unatema madini pasipo mtu kushika sululu na kuchimba. Ameimba nyimbo nyingi kali ambazo katika hali halisi, huwezi kuzitaja zote maana ni nyingi tangu aanze makeke yake kwenye game.

Baada ya kuwa alipotea, baadaye alipoacha matumizi ya madawa ya kulevya, alichukuliwa na Kampuni ya QS Mhonda J Entertainment kwa ajili ya kufanya naye kazi kama msimamizi.

Kampuni hii imemudu kufanya naye kazi kwa mafanikio makubwa, ingawa siyo kama ambavyo mashabiki wanaofahamu hasa uwezo wa msanii huyu walitegemea. Ameingia studio na ametoa video kali ambazo wadau wamezikubali.

Lakini katika hali isiyotarajiwa, hivi karibuni watu wanaodaiwa kuwa wazazi au ndugu zake wamejitokeza katika chombo kimoja cha habari na kutoa madai ya kumlaumu mdhamini huyo kwa kushindwa kutekeleza baadhi ya vipengele vya mkataba walioingia, kitu ambacho wao wanakiona siyo sawa.

Q Chief

Jambo hili limeshangaza kidogo, kuona ndugu wakienda kwenye media kumlalamikia mdhamini, maana ilitarajiwa Q Chillah mwenyewe ndiye ajitokeze hadharani ili kupinga namna mkataba wake unavyotekelezwa kwa sababu yeye anajua wapi ni sawa na wapi si sawa.

Kinachoonekana ni kuwa yeye mwenyewe ndiye ametoa siri za mkataba wake kwa ndugu hao, maana kama siyo yeye isingekuwa rahisi kujua maana mkataba siku zote huwa ni siri. Kama siyo hivyo, pia upo uwezekano wa yeye mwenyewe kuwatuma wakatoe madai hayo ili kumshinikiza QS Mhonda atekeleze vipengele vilivyomo.

Huenda kuna mantiki kwa ndugu hao, lakini kwangu sioni kama jambo hilo ni sawa kwa sababu kitakachomfanya mdhamini wake kutekeleza matakwa yote ya mkataba, ni kuishi pia kwa kazi anazofanya.

Kama mashabiki hawapokei kazi zake kwa kasi iliyotarajiwa, ni wazi kuwa hata mafao nayo yanapaswa kuja kwa mtindo huo, kwa sababu huwezi kutegemea mavuno makubwa kwa mazao yasiyotunzwa vyema.

Rai yangu kwa Q Chillah ni kuongeza ubunifu katika kazi zake kwanza, ili abebwe na uwezo wake badala ya kumtegemea mtu mwenye fedha zake, ambadilishie maisha kwa kazi ambazo sokoni haziuzi.

Dully Sykes

Comments are closed.