The House of Favourite Newspapers

Ney ‘Asanda’ kwa Madee

Madee

Na ALLY KATALABULA| IJUMAA WIKIENDA| OVER ZE WEEKEND

 

RAPA asiyeishiwa vituko kunako Muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kidizaini kama amelimaliza bifu ‘amesanda’ kwa hasimu wake, Hamad Ally ‘Madee’ baada ya kumfagilia kuwa ni miongoni mwa wasanii wachache wa Hip Hop wanaofanya vizuri kwa sasa.

Ney Wa Mitego

Akipiga stori na Over Ze Weekend, Nay alisema licha ya kwamba Madee ni hasimu wake kimuziki lakini anakubali kazi za mwanamuziki huyo asiyechuja kwa kuwa anajua kusoma alama za nyakati.

Madee na Warembo

“Ni msanii mzuri anajitahidi, anatoa ngoma kali, anajua kuandika vizuri na hata melodi zake ziko poa, kimsingi anajua kusoma alama za nyakati katika kila zama za muziki huu wa Bongo, nikipewa nafasi ya kumzungumzia Madee nafikiri hilo ndilo ninaloweza kusema,” alisema Nay wa Mitego.

Comments are closed.