The House of Favourite Newspapers

Q- Chillah Alalamikia Mkataba wa QS

NA ALLY KATALAMBULA | RISASI JUMAMOSI | MIKITO NUSUNUSU

MWANAMUZIKI  mkongwe kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Aboubakar Katwila  ‘Q-Chillah’ amefunguka na kulalamika kuwa katika makosa makubwa aliyowahi kuyafanya basi ni kusaini mkataba na Lebo ya QS ambao ni mbovu kuliko wowote ule ambao amewahi kuona.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Q-Chillah   alisema mkataba alioingia na Qs ambao alisaini akiwa hayuko timamu kiakili kutokana na kwamba nyakati hizo alikuwa akipambana kutoka kwenye matumizi ya madawa haramu ya kulevya ulikuwa mbovu na ndiyo ameushtukia sasa hivi.

“Mkataba niliosaini na QS ni mkataba ambao una vipengele vilivyojaa urasimu, kipindi naingia nao mkataba ule nilikuwa niko kwenye mapambano ya kutoka kwenye madawa haramu ya kulevya akili haikuwa sawa hivyo jambo kubwa ambalo nitashughulika nalo mwaka huu ni kuvunja mkataba huo na kutafuta mahali pengine ambapo patakuwa sahihi,” alisema Q-Chillah.

Comments are closed.