The House of Favourite Newspapers

G Nako auza video Sh. 300

Na WAANDISHI WETU| GAZETI LA UWAZI| SHOWBIZ

MKALI wa kurap Bongo, George Mdemu ‘G Nako’ amefunguka kuwa baada ya kufanya biashara ya kuuza nyimbo zake kwa muda mrefu katika mfumo wa audio mitandaoni sasa ameingia rasmi kuziuza kwenye mfumo wa video ili kutanua soko la muziki wake duniani.
Akichonga na Uwazi Showbiz, mkali huyo anayefanya poa na ngoma yake iitwayo Go Low aliyomshirikisha Jux huku ikitengenezwa na Prodyuza Lua wa Switch Records alisema video zake zote kwa sasa hazipatikani bure mitandaoni, bali zinapatikana kwa shilingi 300 tu.
“Tumefanya kazi za bure muda mrefu sana, mashabiki wangu watakuwa wanaelewa wazi kuwa kwa muda wote niliokuwa ninafanya kazi video zangu zilikuwa zinapatikana bure mitandaoni, kwa hiyo kwa sasa nimeamua kujiweka kibiashara zaidi na ninaimani nitafanikiwa zaidi,” alisema G Nako.

Comments are closed.