The House of Favourite Newspapers

Sikia Kuhusu Mapacha Hawa!

Picha hii imetumika kama mfano.

Na MWANDISHI WETU| RISASI MCHANGANYIKO| MAKALA

KUNA simulizi nyingi zinazowahusu mapacha, lakini hii ni habari ambayo itakushangaza, utakapobaini kuwa ilitokea huko Los Angeles nchini Marekani katikati ya miaka ya 1960. Mara tu baada ya kuzaliwa, mapacha hao wa kiume walitenganishwa ili waweze kuasiliwa (adoption).

Wazazi wao wapya kamwe hawakuwahi kufahamiana wala kuonana, ingawa kila mtoto aliambiwa kuwa alikuwa na pacha wake. Miaka 40 baadaye, pacha mmoja, James akaamua kuanza kufuatilia ili aweze kumtambua ndugu yake.

Baada ya msako wa muda mrefu, hatimaye alimkuta ndugu yake na akafahamu yafuatayo; Waliomuasili kaka yake, pia walimpa jina la James! Ingawa James hao wawili hawakuwahi kuonana kabla, lakini wote walisomea sheria. Lakini wote pia walikuwa wazuri katika ufundi seremala na uchoraji.

Akina James hao kila mmoja alioa mwanamke aliyeitwa Linda. Kila mmoja alikuwa na mtoto wa kiume, wa kwanza akimuita mwanaye James Allan na wa pili, akiitwa James Alan. Mapacha hao pia kila mmoja alimtaliki mkewe Linda na kuoa mwanamke mwingine, wote wakiitwa Betty na wote walimiliki mbwa aitwaye Toy!

Comments are closed.