×

Lulu Diva: Amber, Gigy Si Saizi Yangu!


STORI: BONIPHACE NGUMIJE | RISASI JUMAMOSI | MIKITO NUSUNUSU

MWANADADA aliyewahi kuwa video Vixen Bongo, Lulu Abassi ‘Lulu Diva’ hivi karibuni amefunguka kuwa kwa sasa hawezi kuwekwa kwenye levo moja na kina Amber Lulu na Gigy Money ambao walikuwa ni wapinzani wake wakubwa kipindi anauza sura kupitia video za muziki.

Gigy Money

Akichonga na Mikito Nusunusu, Lulu alisema ni kweli wapinzani wake wote hao wanafanya muziki kwa sasa kama anavyofanya yeye lakini bado levo zao si kama zake maana yeye yupo chini ya uongozi unaosimamia kazi zake za kimuziki na umemuwezesha kupata kolabo nje ya nchi na Mzimbabwe Jah PPrayzah.

“Kwa sasa kunilinganisha na akina Amber Lulu na Gigy Money ni dharau kubwa, si levo zangu, tazama muziki wanaofanya na muziki wangu.

Amber Lulu

Unaona kabisa nipo mbele na kwa taarifa yao tu nimepiga kolabo na Japlaz yule Mzimbabwe aliyefanya wimbo na Diamond,” alimaliza Lulu Diva.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.