×

Singida United Wakabidhiwa Basi la Sh. Milioni 350

 

UONGOZI wa Klabu ya Singida United, imetoa basi lenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 350 litakalotumiwa na wachezaji pamoja na benchi lao la ufundi katika msimu ujao.

 

 

Singida United ambayo ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda daraja kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao, kesho Jumanne inatarajiwa kuanza kambi ya maandalizi ya msimu huo mkoani Mwanza. Timu zingine zilizopanda daraja ni Njombe Mji na Lipuli FC.

 

 

Mratibu wa timu hiyo, Festo Sanga, amesema: “Uongozi umenunua basi hili lenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 350 ambalo litakuwa likitumiwa na timu popote itakapoenda kucheza mechi zake kwa msimu ujao.

 

 

“Katika maandalizi yetu ya msimu ujao, leo Jumatatu tunakwenda Mwanza na kesho tunatarajiwa kuanza kambo yetu tukiwa huko. Tumepanga kwenye maandalizi yetu kucheza mechi 10, tano ni dhidi ya timu za ndani ya nchi na tano dhidi ya timu kutoka nje ya Tanzania.

 

 

“Katika ishu ya usajili, bado tunaendelea, lakini kwa sasa tuna wachezaji 11 walioipandisha timu, sita tumewasajili kutoka nje ya nchi na wanne ni wazawa tuliowasajili hivi karibuni.”

Leave a Comment