
HATIMAYE mmoja wa washindi wa Shindano la Smart Phone kupitia kipindi cha michezo cha SpotiHausi kinachorushwa na Global TV Online, amekabidhiwa zawadi yake ya simu mpya aina ya Tecno WX3 leo, katika Ofisi za Global Publishers zilizopo Mwenge Bamaga jijini Dar.
Akipokea zawadi hiyo kwa niaba ya nduguye, George Kipangula ambaye ni kaka wa mshindi, Joseph Kipangula mkazi wa Iringa ameeleza furaha yake baada ya kupokea zawadi hiyo;
“Nimefurahi sana kupokea zawadi hii kwa niaba ya mdogo wangu aliyeshinda smart phone kupitia Shindano la Spoti Hausi, nimeamini kumbe kweli Global TV Online wanafanya mashindano yao bila upendeleo.
“Sikutarajia kama mtu wa Iringa angeshinda hii zawadi, nilidhani pengine washindi wanapangwa, au pengine angetoka Dar, lakini siyo hivyo. Nawaomba watazamaji, wadau na wananchi wote ndani na nje ya nchi kutazama kipindi cha Spoti Hausi na vipindi vingine vya Global TV Online kwani vinaelimisha na kuburudisha pia.

Naye Mratibu wa Shindano hilo ambaye pia ni Meneja wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Global Publishers, Edwin Lindege alisema;
“Shindano ni zuri, na halina ugumu wala hapana upendeleo wa aina yeyote. Kushiriki ni rahisi ingia YouTube, tafuta Global TV Online, ikifunguka Subscribe kwenye batani nyekundu kisha bonyeza alama ya kengele hapo utapata taarifa ya kila kinachoendelea Global TV Online.
“Shindano hili lipo kila Alhamisi wakati wa kipindi cha SpotiHausi kuanzia saa 10:00 hadi saa 11:00, unachotakiwa kufanya ni ku-comment na kuandika namba yako ya simu, ku-like na ku-share link ya kipindi kwa marafiki, mwisho wa kipindi yatachukuliwa majina ya washiriki wote, yataingizwa kwenye droo na mshindi atapatikana huku matukio yote hayo yakionyeshwa live na Global TV Online.

Katika kipindi cha Spoti Hausi cha Alhamisi iliyopita wahindi walikuwa ni Joseph Kipangula mkazi wa Iringa Mjini (aliyechukua zawadi yake leo) ambaye anatumia jina la Mkata Kiu TV pamoja na Chaz Muro ambao walipigiwa simu moja kwa moja na kuulizwa maswali machache yaliyothibitisha uhalali wa ushindi wao na kisha kupewa maelekezo ya namna ya kuzipata zawadi zao.
Kipindi cha Spoti Hausi huruka kila siku ya Alhamisi, kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa kumi na moja kamili jioni. Kutazama kipindi hiki, ingie YouTube na kisha andika Global TV Online na hapo utapata fursa ya kutazama kipindi hiki bora kabisa cha michezo, kikiendeshwa na wachambuzi mahiri na wabobezi wa masuala ya michezo na burudani, wakiongozwa na Saleh Ally ‘Jembe’.