×

PICHAZ: Sugu, Msigwa Walivyokata Mauno Harusi ya Prof. Jay

Wageni waalikwa wakiingia ukumbini.

 

USIKU wa kuamkia leo ilikuwa ni shangwe kwenye Ukumbi wa Mlimani City wakati wa sherehe ya Rapper nguli wa Bongo ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay’ aliyefunga ndoa jana hiyohiyo Julai 8, 2017  na mpenzi wake Grace katika Kanisa la St. Joseph lililopo Posta ya Zamani Dar.

 

Wabunge Peter Msigwa (wa pili kulia), Sugu (katikati) na wengine wakicheza muziki wakati wa kuingia ukumbini.

 

Katika sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu maarufu kibao wakiwemo wabunge, wasanii wa muziki, filamu na komedi pamoja na viongoizi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa.

 

Prof. Jay akiimba ‘Kamili Gado’ huku akiwa amemshikilia bibie wakiingia ukumbini.

 

Katika kusherehekea harusi hiyo, wakati wa kuingia ukumbini Prof. Jay aliingia akiimba wimbo wake wa ‘Kamili Gado’ huku akiwa amemshikilia mkewe, Bi. Grace, wimbo ambao uliamsha hisia kwa waalikwa wakiwemo wabunge Mch. Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambao walionekana kucheza kwa nguvu zote kumsapoti mbunge mwenzao.

 

Prof. Jay akikamua.

 

Global Publishers ilifanikiwa kunasa picha kadhaa wakati sherehe hiyo ikianza na waalikwa wakiingia ukumbini pamoja na maharusi wenyewe.

 

Mchungaji Peter Msigwa akifnya maombi kabla ya shughuli ya harusi kuanza.

 

Waalikwa wakiwa ukumbini.

PICHA NA RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS

==============

VIDEO: TAZAMA TUKIO ZIMA LA HARUSI YA PROF> JAYA MLIMANI CITY

Leave a Comment