×

SIKU YA DROO KUBWA… MAMBO HADHARANI

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo akikabidhi funguo kwa mshindi wa nyumba awamu ya kwanza, Nelly Mwangosi.

BAADA ya miezi sita ya wasomaji wa magazeti ya Global Publishers kupata kuponi zao na kuzituma kupitia kwa mawakala mbalimbali, uongozi wa kampuni hiyo ya magazeti umetangaza kuwa droo kubwa, ambayo mshindi wake ataondoka na zawadi ya nyumba yenye thamani ya mamilioni ya shilingi, sasa mambo hadharani kwani itafanyika mwezi huu wa tisa.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alisema jana kuwa droo hiyo ilikuwa ichezeshwe mapema, lakini kukawa na vitu vidogovidogo ambavyo vilisababisha zoezi hilo kutofanyika, lakini baada ya kuviondoa, sasa ni wa mamilioni, utampata mwenyewe mwezi huu.

“Ninachoweza kuwaambia wasomaji wa magazeti yetu ni kuwa tumeshamaliza vikwazo vilivyokuwa vinatukabili, droo yetu kubwa itachezwa mwezi huu katika siku ambayo tutawaeleza hapo baadaye kidogo, tuendelee kufuatilia katika kurasa za magazeti yetu tutajua lini hii shughuli itafanyika,” alisema Mrisho.

Kuponi za Shinda Nyumba zikichanganywa wakati wa droo ili kumpata mshindi.

Mrisho aliwataka wasomaji kuendelea kukata kuponi katika magazeti, zinazopatikana katika kurasa za ndani za kila gazeti za Global Publishers ambayo huuzwa kwa shilingi mia tano tu ambayo ni Championi, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani, Uwazi na lile la Ijumaa ambalo huuzwa kwa shilingi elfu moja, lakini likiwa na kuponi mbili.

Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili inafanyika baada ya kuwepo kwa droo ndogo tano zilizochezeshwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ambako zaidi ya wasomaji 30 wa magazeti ya Championi, Ijumaa, Risasi, Uwazi, Amani na Ijumaa Wikienda waliibuka na zawadi za aina mbalimbali zikiwemo pikipiki, televisheni kubwa, simu za kisasa za mikononi, dinner set na ving’amuzi.

Droo hizo ndogo zilifanyika katika maeneo ya Dar Live Mbagala, Manzese Bakhresa, CCM Mwinjuma Mwananyamala na Mabibo Soko la Ndizi, matukio ambayo yalihudhuriwa na mamia ya wasomaji.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa kampuni hiyo kuchezesha bahati nasibu na kutoa zawadi ya nyumba baada ya mwaka jana kufanya hivyo ambapo mjasiriamali kutoka Iringa, Nelly Mwangosi alijipatia zawadi hiyo kubwa kabisa ambayo imebadili kabisa maisha yake ambayo sasa yamekuwa bora zaidi.

Bahati Nasibu hiyo ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na kampuni ya Premier Bet.

NA MWANDISHI WETU

JUMBA LA DHAHABU – 37 & 38

Majonzi Yatawala Kuagwa Kwa Mbunge Mteule Wa Cuf, Bi Hindu Mwenda

Leave a Comment