
Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma, imewaonya viongozi wa umma watakaojaribu kuchepusha mali au madeni yao kwa kuwapa watoto wao wenye umri zaidi ya miaka 18 kukwepa zoezi la uhakiki wa mali zao, unaotarajia kuanza Juni 18, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Juni 11, Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti hiyo, Jaji Mstaafu Harold Nsekela, amesema ni vyema wahusika wote ambao tayari wamepokea barua za uhakiki huo wakawa na nyaraka zote muhimu.
Aidha, akizungumzia uhakiki wa mwaka uliopita Nsekela amesema Desemba 27, mwaka jana zoezi lilifanikiwa kwa asilimia 98 ambapo waliwataka viongozi kurejesha fomu za tamko la rasilimali na madeni na viongozi waliotakiwa kurejesha fomu hizo walikuwa 16,339.