
Mahakama ya Wilaya ya Ngara imewahukumu raia wanne wa Rwanda kwenda jela miaka 20 kila mmoja, baada ya kukutwa na hatia ya makosa manne waliyotenda kwa kuingia nchini mwaka 2016 kinyume cha sheria.
Watuhumiwa hao ni Yauza Faustine(68) mkazi wa Nyarutete, Akizamunga Augustine(52), Kasasila Twagilaelo(37) na Ndikubihimana Oscar(22) wote kutoka maeneo mbalimbali ya Rwanda.
Walikamatwa katika hifadhi ya wanyamapori ya Burigi baada ya kuingia bila kibali cha Mkurugenzi wa wanyamapori.
Kosa la pili ni kuingia nchini bila kibali huku kosa la tatu ni kukutwa na nyara za Serikali ambazo ni nyama za wanyama mbalimbali zenye thamani ya Dola 540,000 za Marekani (Tsh. Milioni 988.8).
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kabuka alisema washtakiwa wote wametiwa hatiani kwa makosa manne hivyo watakwenda jela miaka 20 kila mmoja na kulipa faini ya Tsh. Milioni 3 kila mmoja.