The House of Favourite Newspapers

ANAYEDAIWA KUMUUA MWANAKWAYA GESTI AKAMATWA KANISANI

 

KIJANA anayedaiwa kumuua Mariam Charles (26), mwanakwaya wa Kanisa la AICT, Chang’ombe (anafahamika kwa jina moja la Frank) amekamatwa leo Jumamosi Septemba 8, 2018 wakati ibada ya mazishi ikiendelea baada ya kuonekana akirandaranda nje ya kanisa hilo.

Hii ni kwa mujibu wa mchungaji kiongozi wa AICT  Chang’ombe, Elisha Isebuka kabla ya kuanza kuhubiri.

 

“Wakati  ibada inaendelea mliona baadhi ya viongozi wakitoka. Kijana anayedaiwa kufanya mambo haya alikuwa akizungukia maeneo haya na sasa amekamatwa. Tuviache vyombo vya dola vifanye kazi,” amesema.

 

VILIO TUPU! KUAGWA KWA MWANAKWAYA ALIYEUAWA GESTI – PICHAZ

 

Mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuwa mchumba wa Mariam, baada ya kukamatwa, wananchi walimshambulia kwa kumpiga lakini polisi walimuokoa kwa kufyatua risasi hewani kisha kumpeleka katika Kituo cha Polisi Chang’ombe.

MWANAKWAYA ALIYEUAWA GESTI, FAMILIA YASIMULIA MAZITO – VIDEO

Mwili wa Mariam ulikutwa kwenye nyumba ya wageni ya East London, Buza anakodaiwa alikuwa na mchumba wake usiku wa kuamkia Septemba 5, 2018.

Comments are closed.