×

Yanga: Waleteni hao KMC, Tushamaliza Kazi

YANGA jana iliingia kambini kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya KMC huku ikitamba tayari imekamilisha maandalizi ya kuwafunga wapinzani wao hao.

 

Timu hiyo iliyoingia kambini Nafeland Hotel iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam, inatarajiwa kuvaana na KMC kesho Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

 

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 64 na mchezo wa mwisho uliopita ilishinda bao 1-0 dhidi ya Alliance, lililofungwa na Mrundi, Amissi Tambwe.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Zahera alisema tayari amewasoma wapinzani wake kupitia video tatu za mwisho alizoziona kwenye michezo ya ligi na Kombe la FA waliyocheza hivi karibuni.

 

Zahera alisema, tayari amezijua mbinu, mifumo na wachezaji hatari wa wapinzani wao, hivyo hana hofu ya mchezo huo huku akiwataka mashabiki kuendelea kuichangia timu yao.

Aliongeza kuwa, kwenye mchezo uliopita wa ligi waliocheza na Alliance, baadhi ya wachezaji wake wawili walishindwa kucheza kwa kufuata maelekezo yake na kusababisha wapate ushindi kiduchu wa bao 1-0.

 

“Kwenye mchezo uliopita wa ligi ulikuwa mgumu kutokana na baadhi ya wachezaji wangu kushindwa kucheza kwa kufuata maelekezo yangu na kusababisha mechi iwe ngumu licha ya kushinda bao 1-0.

 

“Nisingependa kuwataja wachezaji hao majina yao, lakini tayari nimewaambia wanapocheza bila ya maelekezo yangu wanaharibu mbinu zangu za ushindi.

 

“Mbinu zangu za mchezo wa KMC tayari nimezimaliza na kilichobaki ni kwa wachezaji wangu kutumia vema maelekezo yangu nikiyokuwa ninawapa mazoezini, nafahamu haitakuwa mechi nyepesi lakini niwaahidi Wanayanga ushindi alisema Zahera