×

Taarifa: Poda za Johnson’s Bay Usitumie, Wala Mtoto Wako

PODA maarufu ya watoto ambayo pia hutumiwa na baadhi ya watu wazima aina ya Baby Johnson kuanzia loti 22318RB haitakiwi kutumika.

 

Imeelezwa kuwa iwapo unayo, basi acha kabisa kuitumia mara moja kwani si salama, hii ni kwa mujibu wa kampuni ya Johnson & Johnson ambayo ilitangaza bidhaa hizo zirudishwe nchini Marekani.

Hata hivyo,  kampuni hiyo inakabiliwa na kesi nyingi kutoka kwa wanawake wanaodai bidhaa zake za talcum zimewasababishia kupata saratani ambapo mpaka sasa kampuni hiyo inakanusha.

 

Mpaka sasa inataka bidhaa 33,000 zilizoingizwa sokoni zirejeshwe kutokana na kemikali iliyo gunduliwa katika bidhaa zilizonunuliwa kupitia mtandao.

 

CHANZO: BBC SWAHILI & CNN