
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imezindua nembo mpya itakayotambulisha na kuonyesha historia ya ukuaji wake tangu ianzishwe miaka 20 iliyopita. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti alisema kuwa, kampuni hiyo ilianzishwa rasmi mwaka 1996 ambapo ilianza kwa kumiliki kiwanda kidogo cha kuzalisha bia jijini Dar es Salaam hadi kufikia kampuni kubwa inayomiliki viwanda vitatu vilivyomo Dar es Salaam, Moshi na Mwanza.
“Nembo mpya ya SBL inasimama ikiwakilisha ubora, ubunifu, utaalamu, urafiki na kujiamini. Nembo hii pia inaonyesha kuwa kampuni yetu inatengeneza bia zake kwa viungo asilia,” alisema Ocitti.
Akizundua uzinduzi huo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocen Bashungwa aliipongeza SBL na kusema kuwa ni kielelezo tosha cha uongozi imara wa kampuni hiyo.

“Tunafahamu kuwa, kutokana na uwepo wa kampuni hii ya SBL, takribani wakulima 400 nchini wanaolima nafaka mbalimbali wanafurahia soko la uhakika la mazao yao ambayo hutumika kuzalisha bia hizi,” alisema Waziri Bashungwa.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SBL, John Ulanga alisema nembo hiyo mpua ionaakisi ukuwaji wa kampuni hiyo na kuongeza kuwa SBL imewekeza pauni za Uingereza milioni 14 katika shughuli zake za upanuzi.
“Uwekezaji huu mkubwa utasaidia kutengeneza ajira mpya zaidi, utaongeza mchango wa SBL kwenye kodi kwa Serikali,” alisema Ulanga. Bia zinazozalishwa na SBL ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Kibo Gold, Guiness pamoja na Senator.
Matukio katika Picha:





Imeandikwa na Neema Adrian/GPL