×

Kifo cha Kwanza cha Corona Nje ya China

MAOFISA wa afya wamethibitishwa kuwa mtu mmoja amefariki kutokana na virusi vya Corona nchini Ufilipino.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa Shirika la Afya, Ulimwenguni WHO, nchini Ufilipino Rabindra Abeyasinghe amewaambia waandishi habari mjini Manila kuwa hicho ni Kifo cha kwanza kuripotiwa nje ya China.

Maafisa wa Ufilipino wamesema mtu huyo alikuwa ni kutoka Wuhan, kitovu cha virusi hivyo nchini China na aliwasili nchini Ufilipino, Januari 21.

 

Alilazwa hospitali mjini Manila na kutengwa Januari 25 baada ya kupata homa, kukohoa na koo kuuma, lakini baadaye alipata kichomi kikali na kufariki baada ya kukaa kwa wiki moja hospitalini.

Leave a Comment