×

Kuiona Yanga vs Simba Buku Saba Tu – Video

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), kupitia kwa ofisa habari wake, Cliford Ndimbo, limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu Bari kati ya Yanga na Simba utakaopigwa Machi 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Katika mchezo huo, kiingilio cha chini ni Sh 7000 ambapo kwa lugha ya mtaani ni buku saba.

Ndimbo alivitaja viongilio vya mchezo huo kuwa ni VIP A Sh 30,000, VIP B Sh 20,000, watakaokaa kwenye viti vya rangi ya machungwa watalipia Sh 10,000, huku mzunguko Sh 7,000.

Ndimbo alisisitiza: “Ni muhimu kwa watu wote kukata tiketi mapema kwa sababu hakutakuwa na mtu ambaye atauziwa tiketi uwanjani, tumekuwa tukipata malalamiko kadhaa juu ya ubabaishaji wa uuzwaji wa tiketi, lakini hiyo yote inatokana na watu kujenga mazoea ya kununua tiketi siku ya mechi.

 

“Sasa ili kulizuia hilo tumepanga kutouza tiketi siku ya mechi pale uwanjani, badala yake watu wanunue tiketi kwenye vituo vitakavyotangazwa.”

 

Yanga watakuwa wenyeji, ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa Januari 4, mwaka huu, ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Leave a Comment