
WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam wa maeneo ya Buza na maeneo ya Kijiwe Samli wamejinasibu kununua kwa wingi magazeti ya Championi na Spoti Xtra ili washiriki kwa wingi Bahati Nasibu ya ‘Baba Lao’ inayoendeshwa na magazeti hayo ambapo mshindi wa droo kubwa ataondoka na gari mpya aina ya Tpyota FunCargo.

Akiinadi Bahati Nasibu hiyo, Mkuu wa Idara ya Masoko ya Global Publishersl, Anthony Adam, amewahamasisha wananchi hao kununua magazeti ya Championi na Spoti Xtra ili kushiriki Bahati Nasibu hiyo kwani nafasi ya kulichukua gari hilo inaweza kwenda kwaao.

Amesema kuwa kadri wanavyoendelea kununua magazeti ndivyo wanazidi kujiongezea nafasi kubwa ya kuwa washindi huku akiwataka kila wanapoona gari la matangazo kujitokeza kwa wingi kukabidhi kuponi ambazo wamekwisha zijaza ama kumpelekea muuzaji wa magazeti aliye karibu nao.

Akiwaelekeza namna ya kushiriki bahati nasibu hiyo, Anthony alisema; “Unachotakiwa kufanya ni kununua magazeti hayo na kukata kuponi iliyopo ukurasa wa pili na kujaza jina lako, namba yako ya simu, anwani yako na umri wako.

Adam ameongeza kuwa mbali na kujishindia gari, kuna zawadi nyingine nyingi kama vile simu za mkononi za kisasa almaarufu kwa jina la Smart Kitochi na nyinginezo ambazo zitatolewa kila mwezi kuelekea kwenye droo hiyo kubwa ya kujishindia gari.

Nunua Gazeti la Championi kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.

JINSI YA KUTUMA:
Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam. Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.

MASHARTI YA KUSHIRIKI:
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.
