Mkurugenzi wa klabu ya Udinese ya Italia, Pierpaolo Marino, amedai bodi ya ligi kuu England (EPL), muda si mrefu, itatoa tamko rasmi la kutangaza kuufuta msimu wa 2019-20 kutokana na janga la virusi vya #Corona.
Akizungumza na gazeti la Sportitalia, Marino ambaye klabu yake inashirikiana hisa na Watford ya England, ametoa habari hiyo ya mshtuko jana usiku, akidai EPL inatarajia kufuata njia ya Ubelgiji, ambao wiki iliyopita walithibitisha kuufuta msimu wa 2019-20, huku Club Brugge, ikipewa Ubingwa.
“Shirikisho la Ubelgiji tayari limeufuta msimu wa ligi kuu, licha ya kupata vitisho vya UEFA. Huko England, EPL wanakaribia kutoa tamko linalofanana na hilo, kwasababu hali inazidi kuwa mbaya sana nchini humo.
“Kiukweli tunatumaini kufurahia tena mpira baada ya virusi vya corona. Haijalishi itachukua muda gani kuisha, sisi tunataka kutoka kwenye eneo hatari. Ninahofia msimu ujao, na sio huu wa zamani,” amesema Marino.
