×

Tanzia: Jaji Augustino Ramadhani Afariki Dunia


Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhani, amefariki dunia leo Aprili 28, 2020, katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu.

 

Jaji Ramadhan aliwahi kutumikia nafasi mbalimbali na kupata vyeo vya juu kiwemo kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Bara na Visiwani mwaka 2002 hadi 2007, pia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar kipindi hichohicho.

 

Pia ni Brigedia Jenerali ambapo alilitumikia Jeshi kabla ya kuitwa katika sekta ya Sheria na kutumikia Mahakama na kuwa Jaji Mkuu Zanzibar.

 

 

Jaji Ramadhani ni Mtanzania wa kwanza kushikilia kiti cha Urais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu tangu kuanzishwa kwa Mahakama hiyo.

 

Alipostaafu ujaji, alipewa kazi ya ukasisi, akatawazwa rasmi kuwa Mchungaji wa Dayosisi ya Kanisa la Anglikana lililopo Mkunazini Zanzibar na hivyo kuitwa “Mchungaji Augustino Ramadhani.” Hadi anafariki alikuwa Mchungaji wa Kanisa hilo.

Kwa taarifa zaidi fuatilia mtandao wetu.

Leave a Comment