Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dkt. Job Asheri Chaula amefariki dunia leo Ijumaa, Mei 8, 2020, asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Chuo Kikuu Ardhi umetangaza msiba wa Mhadhiri wake katika skuli ya Earth Sciences, Real Estate, Business and Informatics (SERBI), Dkt. Job Asheri Chaula kilichotokea leo katika hospitali kuu ya Taifa Muhimbili.
Dkt. Chaula alikuwa mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Tanzania, Jenifer Mgendi ambaye walifunga ndoa mwaka 1998 na kubarikiwa kupata watoto watatu (Jotham, Jeftah na Joan).
Chuo kimesema taarifa za mazishi zitatolewa mipango itakapokamilika. Dkt. Chaula ameacha mke na watoto watatu


