×

Mapokezi Watoto Wa Mondi Bongo Balaa!

 

 

 

DAR: Good news! Ndiyo, kama mambo yatakwenda vizuri, basi usishangae kuwaona watoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tiffah Dangote na Prince Nillan wakiogelea kwenye swimming pool la pale Madale-Tegeta jijini Dar, Gazeti la IJUMAA linakuletea habari yenye matumaini mapya.

 

TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo makini kilicho ndani ya familia ya Diamond au Mondi kimeeleza, baada ya kuwa kwenye sintofahamu ya muda mrefu, sasa hivi mazungumzo yamefikia mahali pazuri kati ya Mondi na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ hivyo amepanga kuwaleta watoto hao Bongo kutoka nchini Afrika Kusini, waje kumuona baba yao, bibi (mama Dangote), babu (Baba D) na ndugu wengine wote.

 

“Sasa hivi wapo kwenye hatua nzuri sana tofauti na ile ya zamani. “Mondi anazungumza na Zari, anawapa watoto simu mara kwa mara na kubwa ndiyo hilo, atawaleta Bongo soon mara tu baada ya janga la Corona kupita,” kilisema chanzo hicho.

Kwenye familia ya baba yao, mapokezi yake yatakuwa ni balaa; si ya kitoto kama yale ya mwana mpotevu aliyechinjiwa mwanakondoo aliyenona, wasomaji wa Biblia wanaelewa hii zaidi.

 

“Wewe si unajua Mondi tena matashtiti yake, watoto hawa hajawaona live muda mrefu, yaani itakuwa furaha na sherehe kubwa sana siku hiyo.

 

“Vyombo vyake vya habari (Wasafi Media) vitarusha tukio hilo, lakini kama hiyo haitoshi, bado media nyingine zitarusha tukio hilo ambalo lina maana kubwa kwa Mondi ambaye amewamisi na kutuhumiwa kuwatelekeza watoto wake, hivyo itakuwa ni bonge la sherehe,” kilisema chanzo hicho.

CORONA TU IKIISHA…

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kinachomzuia Zari kuwaleta watoto hao Bongo kwa sasa ni janga la Corona ambalo limesababisha nchi nyingi kufunga mipaka yake ikiwemo anayoishi Zari, Afrika Kusini.Chanzo hicho kilisema, hata hivyo, familia ya Mondi inaamini mipaka inakwenda kufunguliwa kwani tayari baadhi ya nchi zimeshaanza kufungua shughuli mbalimbali kwa tahadhari, hivyo jambo hilo linakwenda kutimia.

 

“Mungu tu asaidie maana walipanga iwe baada ya Ramadhani na kama unavyojua Ramadhani inaisha wiki ijayo, hivyo itabaki kizuizi tu cha Corona na mambo yakiwa safi, basi watoto wanakuja,” kilisema chanzo chetu ndani ya familia ya Bongo.

MONDI ANASEMAJE?

Gazeti la IJUMAA lilimvutia waya Mondi ili kumsikia anazungumziaje mapokezi ya watoto wake hao aliowamisi kwa muda mrefu, lakini simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa.

WAKO VIZURI

Hata hivyo, kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni kupitia Wasafi TV na Wasafi Radio, Mondi alikaririwa akisema kuwa yupo kwenye mawasiliano mazuri na mzazi mwenzake na siku siyo nyingi watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwalea watoto wao kwa pamoja.

Alisema kuwa, mambo yanakwenda vizuri na hakuna tena ile misimamo ya kisheria ambayo Zari alikuwa anambana Mondi kuhusu watoto hao na mambo mengine ya kifamilia.

 

Siku chache baada ya mahojiano hayo, Mondi alionekana kwenye Instagram akizungumza moja kwa moja na watoto hao kwa njia ya simu, jambo ambalo liliashiria matumaini mapya!Kama hiyo haitoshi, mapema wiki hii aliposti tena video ya watoto hao akiwasifia ambapo muda mfupi baadaye ilikuwa imetazamwa na wafuasi wake zaidi ya 566,000 kwenye ukurasa wake wa Instagram.

BABA MONDI ANENA

Gazeti la IJUMAA pia lilizungumza na baba mzazi wa Mondi, Abdul Jumaa ‘Baba D’ ambapo alisema anafurahi kuona Mondi na Zari wanamaliza tofauti zao kwani ni jambo ambalo hata yeye alikuwa anatamani litokee.“Unajua inafika mahali hata kama wazazi mlikuwa na tofauti zenu, lakini kwa kuwa kuna watoto, ni vizuri sana kuwatendea haki ili nao wapate malezi ya pande zote mbili,” alisema Baba D ambaye amekuwa hafichi kueleza namna anavyomkubali Zari.

 

TUJIKUMBUSHE

Februari 14, 2018 ndiyo ilikuwa siku ya mtikisiko mkubwa zaidi kwa Mondi na Zari. Zari alitangaza rasmi kumwagana na Mondi kwa kile alichodai kuwa staa huyo wa Wimbo wa Jeje alishindwa kujiheshimu na kuchepuka mara kwa mara.Baada ya siku hiyo, kilichofuata hapo ilikuwa ni uadui mwanzo mwisho. Ilifika mahali, Mondi aliwekewa ngumu hata kwenda nyumbani kwa Zari (Sauzi) kuwaona wanaye tena kisheria kabisa. Kama hiyo haitoshi, inaelezwa kuwa Zari aliamua kuhama kwenye nyumba aliyonunua Mondi huku akimchana mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni mwanaume asiyefaa.

Stori:MWANDISHI WETU, Ijumaa

Leave a Comment