×

Rais Zuma Ammwaga Mchumba wa Miaka 25

ALIYEKUWA Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, anadaiwa kuwa ameachana na mchumba wake mwenye miaka 25, Nonkanyiso Conco.

Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kuwa wawili hao waliachana mwaka jana na Conco amehama kutoka kwenye nyumba aliyokuwa amepangishiwa na Zuma jijini Durban.

Vyanzo vya karibu na wawili hao vinadai kuwa Conco aliambiwa afanye kuachana huko kuwe siri. Walinzi katika nyumba aliyokuwa akiishi mwanadada huyo wamesema kuwa alihama Disemba 2019, mara baada ya kutembelewa na Zuma kwa mara ya mwisho.

Baba yake, Fartescue Conco, amethibitisha binti huyo kuhama na amesema sasa anaishi na mama yake.

Conco aligonga vichwa vya habari mapema mwaka huu kufuatia chapisho lake katika mtandao wa Instagram kutafsiriwa kuwa anamlea mwanaye bila usaidizi wa baba ambaye inasemekana ni Zuma.

 

Leave a Comment