×

Chama Atua Simba, Sasa Azam FC Kazi Wanayo

CLATOUS Chota Chama, maarufu kama Mwamba wa Lusaka, ‘Jembe la Kazi’ ndani ya Simba, limetua rasmi jana kwa ndege akitokea nchini Zambia ambako alikuwa kwa ajili ya mapumziko ya lazima yaliyotokana na kuibuka kwa Virusi vya Corona.

 

Chama aliibuka nchini Zambia baada ya Serikali kusitisha masuala ya michezo Machi 17, alichelewa kurudi kutokana na mipaka ya Zambia kufungwa jambo ambalo liliwafanya Simba kuwasiliana na ubalozi wa Zambia. Akiwa uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, majira ya saa saba mchana, Chama alipokelewa na Mratibu wa Simba, Abbas Selemani.

Chama anaungana na majembe mengine ya kazi mawili ambayo nayo pia yalikuwa nje ikiwa ni pamoja na Francis Kahata aliyekuwa Kenya na Meddie Kagere aliyekuwa Rwanda. “Ilibidi nirudi Jumatatu (leo) ila ratiba ya ndege ya Ethiopia Airline ambayo nilipanda ilibadilishwa, kwa hiyo safari ya kesho (leo) ikawa ni leo (jana) ,” alisema Chama alipozungumza na Championi Jumatatu baada ya kutua Dar.

 

Majembe haya yote kiujumla yamehusika kwenye jumla ya mabao 43 ambapo Chama amefunga mabao mawili na pasi saba za mabao, Kagere amefunga mabao 19 na pasi tano za mabao huku Kahata akifunga mabao manne na pasi sita za mabao jambo linaloongeza mzigo mzito kwa Azam FC iliyo chini ya Aristica Cioaba zitakapokutana kati ya Juni 30 hadi Julai Misi kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Uwanja wa Taifa.

Mchezaji mmoja kwa sasa ndiye amebaki kurejea nchini kujiunga na wenzake ambaye ni Sharaf Shiboub raia wa Sudan, jitihada za kumpata zinaendelea huku sababu kubwa ya kuchelewa kwake kurudi ni mipaka ya Sudan kufungwa mpaka sasa kutokana na janga la Virusi vya Corona.

 

Simba ilianza mazoezi tangu Mei 27 kwenye uwanja wao wa Mo Simba Arena uliopo Bunju kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho, Juni 14 itamenyana na Ruvu Shooting, Uwanja wa Taifa.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA NA JOEL THOMAS

Leave a Comment