LEO Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendele Freeman Aikael Mbowe, amekubali kutia nia ya kugombea uraisi baada ya wazee wa chama hicho kuamua kumchukulia fomu. Wazee hao wa mkoa wa Dar es salaam walioambatana na vijana walifika nyumbani kwake wakiwa na barua ya kutia nia, waliyoiandika kwa niaba ya Mbowena kumtaka aisaini ili ipelekwe kwa katibu mkuu wa chama hicho.