×

Mshindi Baba Lao: Nilidhani Matapeli, Leo Nimekabidhiwa Gari – Video

Mshindi wa gari mpya aina ya Toyota FunCargo kutoka promosheni ya #ChomokaNaGari2020 #BabaLao, Didas Marik Munishi (wa pili kulia) wa jijini Dar es Salaam.

 

HATIMAYE lile Shindano la promosheni ya  #ChomokaNaGari2020  #BabaLao, aina ya Toyota FunCargo limetamatika baada ya mshindi wa bahati nasibu hiyo, Didas Marik Mushi, mkazi wa Jiji la Dar es Salaam kukabidhiwa zawadi hiyo.

Amekabidhiwa zawadi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa kupitia magazeti bora ya michezo nchini, Championi na Spoti Xtra leo Jumatano, Julai 15, 2020, na Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara, katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi zawadi hiyo, Didas amesema, “Wakati nacheza shindano hili sikujua kama nitashinda, siku ya droo kubwa ya fainali nilipopigiwa simu na kuambiwa nimeshinda, nikakata simu, kila wakipiga ninakata nikijidhani kuwa ni matapeli wa mjini wanataka kuniibia, baadaye mke wangu akasema si ulikuwa unacheza hiyo bahati nasibu? Basi wasikilize, kama ni matapeli utajua.


“Nikapokea simu wakanieleza nimeshinda lakini wataniambia utaratibu wa kuchukua zawadi yangu, nikasema yaleyale, utapeli tu huu, nitaamini kama wakinikabidhi zawadi yangu, zikapita wiki mbili  bila kupigiwa simu wala kuambiwa chochote kuhusu zawadi, nikajisemea huenda ni matapeli tu. Lakini leo nimeamini kwamba Global Publishers hawana longolongo, nimekabidhiwa gari mpya, siamini aisee.

“Nilikuwa nikinunua magazeti mara kwa mara na kukata kuponi, lakini sikuwahi kuamini kama nitashinda. Pale kijiweni kwetu watu wakawa wanasema kama tupo watu wengi sana hapa Kariakoo na hakuna mtu aliyekufa kwa corona hizi ni stori tu huwezi kushinda.

“Hapa Global Publishers sijawahi kufika ndiyo mara yangu ya kwanza leo, wala simjui mtu yeyote  hapa lakini nimeshinda na nimekabidhiwa zawadi, namshukuru sana Mungu. Global Publishers wanafanya mashindano yao kwa haki na kweli kabisa  tena bila upendeleo wowote.

“Lakini leo nimeamini kumbe ukicheza promosheni za @GlobalPublishers unashinda, mpaka wazazi wangu nyumbani Moshi wananipigia simu ‘njoo’, wanataka walione gari ili waamini kama kweli nimeshinda, nawashauri Watanzania washiriki mashindano ya Global Publishers ni ya kweli kabisa hayana ujanja ujanja,” amesema Didas.


Promosheni ya Chomoka na Ndinga ilikuwa ikiendeshwa tangu Feb. 27, 2020,  kupitia magazeti bora na yanayoongoza kwa habari za michezo nchini, #Championi & #SpotiXtra.

Leave a Comment