×

Wanahabari Washiriki Maandamano Kumpinga Rais

WAFANYAKAZI wa Shirika la Habari la Belarus wameacha majukumu yao na kujiunga na maelfu wa waandamanaji kutaka Rais wa nchi hiyo, Alexander Lukashenko kujiuzulu.

 

Mmoja wa wafanyakzi hao akihojiwa na Kituo cha Interfax amesema wanaandamana kuungana na takriban wafanyakazi 100 ambao wamekusanyika katika makao makuu yasShirikia hilo huko Minsk.

 

Belarus imekumbwa na maandamano makubwa tangu Jumapili iliyopita wakati rais wa nchi hiyo alipotangazwa mshindi katika uchaguzi ambao mpinzani wake anasema haukuwa wa haki.

 

Vyama vya upinzani viliitisha maandamano kwa nchi nzima kuanzia Jumatatu baada ya maelfu ya wafanyakazi katika kiwanda kinachomilikiwa na serikali kuweka nyenzo chini na kuanza maandamano.

 

Aidha, kwa mujibu wa taarifa, wafanyakazi wa shirika la habari la serikali wameandika maombi maalumu yenye matakwa kadhaa kwa uongozi wao ikiwemo kutaka kuacha kuchuja taarifa na kutambua  kwamba uchaguzi uliofanyika haukuwa halali.

Leave a Comment