
Zaidi ya watu 50 wanahofiwa kupoteza maisha, baada ya kufukiwa na kifusi wakiwa kwenye machimbo ya dhahabu katika eneo la Kamituga, Kivu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Gavana wa jimbo la Kivu Kusini, Theo Ngwabije amethibitisha taarifa hizo, Septemba 12, 2020 na kusema juhudi za kuwanasua watu hao waliokwama chini ya ardhi baada ya mgodi kuporomoka kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo.
Meya wa Kamituga, Alexandre Bundya ametangaza siku mbili za maombolezo na kueleza kwamba wengi wanaohofiwa kupoteza maisha, ni vijana wadogo wanaofanya kazi ya kutafuta dhahabu kwenye machimbo hayo.