Mgombea wa kiti cha urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli jana aliwaomba wananchi wamchague tena amalizie awamu yake ya pili ili azidi kufanya maendeleo zaidi ya aliyoyafanya.
Dkt. Magufuli aliwaomba wanachi ridhaa hiyo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar ambapo katika mkutano huo, aliwanadi wagombea ubunge pamoja na udiwani katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar.
Dkt. JPM aliwaasa wakazi wa jiji la Dar kuwachagua wabunge hao ili akashirikiane nao vizuri katika kuzidi kuriboresha jiji la Dar ambalo ndani ya kipindi cha miaka mitano ameshafanya mambo makubwa ya kimaendceleo ambayo hayajawahi kutokea.







