



Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wamefika nyumbani kwenye familia ya watu wa tano ya , Edward Jeremiah Katema waliopoteza maisha katika ajali ya moto kwa ajili ya kutoa pole na kuendelea shughuli nzima za maombolezo.
Katemi akizungumzia chanzo cha vifo hiyvyo alisema kuwa ni kutokana na hitilafu ya umeme uliopelekea kuunguza nyumba yao na kusababisha vifo vya wanafamilia hiyo.
Amesema kuwa wakati akitokea katika shugghuli zake majira ya saa nne usiku ndipo alikutana na janga hilo la moto ambapo walifanya juhudi za kuwaokoa lakini kwa bahati mbaya ilishindikana kutokana na kuwa tayari walikuwa wameumia sana lakini walifanya juhudi za kuokoa uhai wao kwa kuwapeleka hospitalini lakini walipoteza maisha.
Akizungumzia taratibu za mazishi ,Jeremiah amesema taratibu za kuhifadhi miili hiyo inaendelea na lakini taratibu za awali wanatarajia kusafirisha miili hiyo hadi Buchosa-Sengerema Mwanza katika kijiji cha Sukuma kata ya Bukokwa.