×

Zari Ampiga Chini King Bae Wake wa Sauz

MREMBO na mwanamama Zari the Boss Lady amethibitisha kuachana na mwanaume wake aliyemtambulisha mtandaoni kama ‘King Bae’ ambaye alifikia hadi hatua ya kumvisha pete ya uchumba.

Baada ya Zari kuachana na Diamond, Februari mwaka 2018, na hii ni baada ya Zari kutangaza jambo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, kwamba msanii huyo amekuwa akimsaliti kwa kuwa na wanawake wengine,    Zari alikaa kwa muda kidogo ndipo akaweka wazi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume huyo ambaye hakuwahi kumuonyesha Sura.

 

Zari amesema kuwa ni kweli mwanamme huyo alikuwepo na wala haikuwa kiki lakini kuna vitu kati yao vilitokea hadi kupelelea mahusiano yao kuvunjika.

Kwa takribani wiki moja sasa Zari amekuwa kwenye  stori kuu za burudani hapa nchini kutokana na ujio wake na watoto wake, Tiffah na Nillan, aliowaleta kumuona baba yao mzazi, msanii Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Leave a Comment