×

Mwanasayansi wa Iran Aliuawa kwa ‘Remote-Control’

MKUU wa masuala ya usalama wa Iran, Ali Shamkhani, amesema  washambuliaji  walitumia kifaa cha kielekroniki  wakati gari la mwanasayansi  Fakhrizadeh lilipofyatuliwa mashariki mwa mji mkuu Tehran.

 

Shamkhani alikuwa akizungumza katika mazishi ya mwanasayansi huyo ambaye Israeli ilimshutumu kwa kusaidia kisiri kutengeneza silaha za nyuklia.

 

Israel haijatoa kauli yoyote wazi kuhusu madai ya uhusika wake, Iran inaamini kuwa Israel na kikundi cha upinzani walitumia silaha ya kielektroniki (remote control) kumpiga risasi mwanasayansi wa ngazi ya juu wa nyuklia, Mohsen Fakhrizadeh, Ijumaa Novemba 25 mwaka huu.

 

Katika miaka ya 2000, Fakhrizadeh alikuwa na mchango mkubwa katika mpango wa nyuklia wa Iran, lakini mwanasayansi huyo wa serikali amekuwa akisisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia wote ni wa amani.

 

Iran imekuwa ikiwekewa vikwazo na mataifa ya Magharibi kwa lengo la kuizuia kutengeneza silaha za nyuklia.

Leave a Comment