×

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi Kifo cha Nsekela

RAIS Dokta John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma, Harold Nsekela aliyefariki leo Desemba 06, 2020 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

 

Katika taarifa iliyotolewa kwa umma na Mahakama ya Rufani imeeleza kuwa Jaji Nsekela amefariki asubuhi jijini Dodoma baada ya kuugua kwa muda mfupi na kwamba taarifa zaidi kuhusu msiba na taratibu za mazishi zitatangazwa baadaye.

 

Jaji Nsekela aliteuliwa kuwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Desemba 2016, wadhifa aliokuwa nao mpaka alipofariki dunia leo asubuhi.

Leave a Comment