
KIKOSI cha Yanga kilitarajiwa kuwasili Shinyanga jana kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Mwadui FC huku Kocha Mkuu Cedric Kaze akionyesha hataki utani kwa kuanza na dozi ya mazoezi wakiwa mkoani hapo.
Yanga ikiwa kileleni katika Ligi Kuu Bara kwa kuwa na pointi 34, imepangwa kukipiga dhidi ya Mwadui FC, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Kambarage.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema mara baada ya kikosi chao kuwasili Mwanza salama kwa usafiri wa ndege walichukuliwa na basi la timu kuelekea Shinyanga ambapo kocha aliamua kuwapa dozi mara baada ya kuwasili Shinyanga.

“Kikosi kinaendelea na mazoezi leo jioni (jana) katika Uwanja wa Freshoo kutokana na mapendekezo ya kocha Kaze, wachezaji hawatakuwa na muda wa kupumzika wataendelea na mazoezi baada ya kufika ili kujiimarisha , hatuna majeruhi zaidi ya Carlinhos ambaye anaendela na matibabu,” alisema Bumbuli.
NA Khadija Mngwai, Dar es Salaam