×

China Yaisamehe DR Congo

SERIKALI ya China imeisamehe Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo sehemu ya deni inaloidai, ili taifa hilo liweze kupambana na janga la virusi vya corona.

 

Waziri wa Kigeni wa China, Wang Yi amesema china imeisamehe Kongo dola milioni 28, wakati wa ziara yake katika taifa hilo la Afrika wiki hii.

 

Aidha Wang amesema China itaisaidia zaidi Kongo kwa kuipa dola milioni 15 ambazo zitatumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo. China ni mwekezaji mkubwa nchini humo.

 

Watafiti wa Kimarekani wanakadiria kuwa China imeikopesha Kongo zaidi ya dola bilioni 2.4 katika miongo miwili iliyopita.

 

Tangu alipogunduliwa mgonjwa wa kwanza mwenye virusi vya corona nchini humo mnamo Machi 10, Kongo imeripoti maambukizi mengine 18,738 na vifo 610.

Leave a Comment