×

Wizara Yahimiza Watanzania Kufanya Utalii wa Ndani

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, amewataka wananchi kuweka utaratibu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na siyo kuwaachia wageni kutoka nje.

 

 

Ametoa wito huo  kwenye kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika jijini Mwanza ambapo amesema ni vema kila mtu kupenda kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

 

 

” Watanzania tupo milioni kwa sasa lakini ukiangalia idadi ya watu wanaoingia kwenye hifadhi zetu na kuangalia utalii ni wachache kuliko idadi ya watu waliopo nchini, na hali hii inaonyesha sisi siyo wazalendo. hivyo ni vema tupende utalii wa kwetu wa ndani,” amesema. na kuongeza kwamba  ugonjwa wa corona umesababisha watalii kutoka nje kupungua kuja nchini kutembelea mbuga zetu japo hali siyo mbaya.

 

“Tulikuwa tukitegemea sana watalii kutoka nje lakini kutokana na ugonjwa corona walisita kuja lakini mwezi Desemba mahotel yote yalijaa watu walijitokeza kutembelea mbuga zetu na kujionea wanyama waliopona tunaendelea kuhamasisha watu wafanye utalii wa ndani ni lazima tupenda vyetu vya ndani.

 

 

Hata hivyo alisema kutokana na barabara kuchangia kwa asilimia kubwa ongezeko la watalii nchini
ni vema wakala wa barabara vijijini na mjini (TARURA) kuona umuhimu kuzitengeneza ili kusaidia kupitika kwa urahisi.

 

 

“Barabara zikiwa hazijatengenezwa vizuri inakuwa changamoto kupitika, hivyo ni vema wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) kuona umuhimu wa kizitengeneza na ikiwezekana kuongeza bajeti ili kusaidia kwenye matengenezo hayo na ziweze kupitika ili zitasaidia kuvutia watalii na kufika eneo husika kwa urahisi na kwa wakati,” alisema Masanja.

Na Leah Marco, Mwanza

Leave a Comment