×

AstraZeneca Zilizotumwa Afrika Zime-Expire

Taarifa imetolewa kwamba chanjo za corona (Covid-19) zilizotumwa kwa nchi 13 barani Afrika zimepita tarehe ya mwisho ya matumizi, lakini bado zinaweza kutumiwa kwa kuwa muda wake halisi wa matumizi ni miezi 3 zaidi.

 

 

Katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na Kituo cha Kiafrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC), ilibainishwa kuwa tarehe ya mwisho ya matumizi ya dozi 925,000 za chanjo ya Oxford / AstraZeneca, ambazo zilitumwa kwa nchi 13 za Afrika katikati ya mwezi Machi, ilikuwa ni Aprili 13.

 

 

Taasisi ya Serum ya India ambayo inazalisha chanjo hiyo, iliiarifu Afrika CDC kuwa muda wa chanjo ni miezi 3 zaidi na ilisisitizwa kuwa chanjo zinaweza kutumika hadi Julai 13, 2021.

 

 

Baadhi ya nchi barani humo zilielezea wasiwasi wao kuhusu tarehe ya kumalizika kwa matumizi ya chanjo zilizopokewa kama misaada kutoka Umoja wa Afrika.

Leave a Comment