×

Mabadiliko Polisi: Mambosasa Apelekwa Dodoma, Wambura Dar


SACP Lazaro Mambosasa ametakiwa kuhama kutoka kuwa Mkuu wa Polisi kanda Maalum Dar, na kwenda kuwa Mkuu wa Oparesheni UPEL Dodoma.

 

Polisi wengine waliohamishwa ni SACP Camilius Mongoso Wambura ambaye anatoka Dodoma na kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.

 

ACP Daniel Shillah amehamishiwa Dar na atakuwa Mkuu wa Upelelezi. ACP Longinus Tibishibwamu atakuwa Kamanda Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mara.

 

SSP Optatus Maganga amehamisha kutoka kuwa OCD Makete kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Njombe. SP Vitus Marekani atakuwa OCD wilaya ya Makete.

Leave a Comment