×

Rais Samia Aongoza Viongozi Kuaga Mwili wa Mzindakaya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho katika Jeneza lenye mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya mara baada ya Misa ya kumuombea Marehemu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay mkoani Dar es Salaam leo tarehe 09 Juni 2021.

Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 9, 2021 ameongoza viongozi kuaga mwili wa Mwanasiasa mkongwe marehemu Chrisant Majiyatanga Mzindakaya katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Rais Samia akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Misa ya kumuombea Marehemu Mzee Chrisant Majiyatanga Mzindakaya iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay mkoani Dar es Salaam leo tarehe 09 Juni, 2021.

Leave a Comment