×

Rick Ross Atoboa Siri Ya Ndevu Zake

rickross2013RAPA mwenye sauti yenye ujazo wa kutosha, anayekimbiza kwa sasa kwenye gemu la Hip Hop kwa Ngoma ya Sorry, Rick Ross ‘Rozee’ hivi karibuni katika mahojiano na Radio Westwood ya Marekani alitoboa siri ya ndevu zake kuwa kila akizinyoa hutumia mwezi mmoja na nusu kurudi katika hali yake.

Rozee aliyenogesha kwa michano kila mara kwenye kipindi hicho alifunguka hilo ikiwa ni jibu la swali aliloulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho aliyependa kufahamu juu ya matunzo na kukua kwake.

“Mara kwa mara huwa nazipunguza na kuzifanya zionekane ziko sawa siku zote katika muonekano wa ubosi, lakini hata nikizinyoa hazichukui zaidi ya mwezi mmoja na nusu kukua na kurudia katika hali yake,” alisema Rozee.

Leave a Comment