
Tanzia: Mchambuzi nguli wa soka Tanzania, Mwalimu Alex Kashasha (64) amefariki dunia leo Alhamisi, Agosti 19, 2021 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na www.globalpublishers.co.tz, mtangazaji wa TBC, Enock Bwigane ambaye amekuwa akitangaza pamoja na Mwl. Kashasha katika kipindi cha michezo cha TBC amethibitisha kutokea kwa msiba huo.
Kashasha alikuwa mtumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) hadi umauti ulipomfika.
Taarifa zaidi tutaendelea kukujuza.